Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Cop 26: Wanaharakati vijana kutoka Afrika wataka dunia ifanye maamuzi sahihi
Viongozi kutoka maeneo mbalimbali duniani wameudhuria mkutano wa 26 wa mabadiliko ya tabia nchi huko Glasgow, Scotland. Mkutano huo unaanza Oktoba 31 mpaka Novemba.
Mkutano huu unahudhuriwa na wawakilishi kutoka mataifa 200 lengo likiwa ni kuweka mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi mpaka 2030.
Dunia imeshuhudia mabadiliko makubwa ya hali ya hewa - kwa kuwa na mafuriko, ukame haswa katika maeneo ya Afrika. Wanaharakati vijana kutoka barani Afrika wanaeleza namna jamii yao ilivyoathirika na wanatuma ujumbe kwa viongozi wa dunia katika COP26.