Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hukumu ya nadra yatolewa Uhispania dhidi ya malezi ya mbwa kwa wapenzi waliotengana
Jaji nchini Uhispania ametoa ruhusa kwa wapenzi walioachana kumtunza kwa pamoja mbwa ambaye walikuwa wakiishi naye.
Wapenzi hao walienda mahakamani wakitaka hakimu kuamua nani ana haki ya kuishi na mbwa huyo.
Mahakama ya Madrid ilizingatia kwamba pande zote mbili zinawajibika kumtunza mbwa huyo.
Wakili aliyepeleka kesi hiyo mahakamani , alisema hukumu hiyo ilikuwa mpya.
Kwa sasa Uhispania inatayarisha sheria mpya ili wanyama wasichukuliwe tena kama vitu na watambuliwe kisheria kuwa viumbe hai.
Hali hii inaweza kumrahisishia mume/ mke kuomba ulezi wa pamoja wa mnyama anayempenda baada ya kutengana.
Lakini Lola García, kutoka kampuni ya sheria na wanyama, akaleta kesiiliyopelekwa mahakamani chini ya makubaliano ya mwaka 1987 ya Ulinzi wa Wanyama wa nyumbani , ambao Uhispania iliidhinisha mwaka wa 2017.
Alisema hii ni hukumu mpya kwa kuwa mteja wake ataweza kujitangaza kuwa mmiliki na mlezi msaidi wa mbwa wao Panda.
Mkataba wa kuasiliwa kwa Panda, malipo ya huduma zake na picha zinawaonesha kuwa wao ni familia, sawa kabisa kama picha ya familia ya wazazi na watoto wao" zilikusanywa kama ushahidi , bi García alisema kwa mujibu wa RTVE.
Jaji alitoa hukumu hiyo kulingana na ushahidi ambao umetolewa unaonesha uhusiano wa kimaadili kati ya mlalamikaji na mbwa unastahili ulezi wa kisheria.
Panda atakuwa ana chaguo la kukaa mwezi mwezi kwa wapenzi hao walioachana.
Sheria za ulezi wa mbwa kisheria duniani kote
Nchini Uingereza, mbwa wana haki kisheria kama vitu visivyo na uhai sawa na magari, nyumba au vitu vingine vya kibinafsi.
Hukumu za kesi za ulinzi wa mbwa zinazingatia kujua mmiliki mmoja tu.
Nchini Australia, sheria inataka mahakama kupata maeneo ambayo wanyama wanatunzwa mara baada ya wanandoa waliokuwa wanawalea kuachana.
Ufaransa ilibadilisha sheria ya wanyama wa nyumbani mwaka 2014 kwa wanyama kuzingatiwa kuwa"viumbe hai na wanaohisi" badala ya "bidhaa zinazohamishika"
Hali hiyo inamaanisha kwamba wanandoa wanaoachana wanaweza kupigania haki ya pamoja katika kesi za talaka.