Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tazama jinsi Mtanzania huyu anavyojitolea kuwavusha watu barabarani
Pengine linaweza kuwa jambo geni kwa raia ambaye si polisi kuongoza magari kwaajili ya kuhakikisha usalama wa wananchi barabarani.
Wananchi wanavuka salama na waendesha vyombo vya moto kama Pikipiki, magari makubwa na madogo wote wanatumia vizuri barabara hasa majira ya asubuhi na jioni muda ambao watu wengi huwa na pilikapilika za kuwahi kwenye shughuli zao na wanafunzi kuwahi shuleni.
Hekaheka hizo zimepelekea kijana mmoja kujitokeza na kuongoza magari na watembea kwa miguu ili kila mtu apate nafasi ya kuitumia barabara vizuri.
Je ungependa kufahamu shujaa huyu anapitia masaibu gani?
Ungana na Frank Mavura katika taarifa hii;