Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uganda: 'Ilibidi nivue nguo kuthibitisha jinsia yangu'
Cleopatra Kamburu anasema ilikuwa aibu kutakiwa kuvua nguo zake ili kuonyesha yeye ni nani. Uganda imetoa kitambulisho cha kwanza kwa watu waliokumbatuia jinsia tofauti na waliozaliwa nayo(Transgender)
Kwa neno la kiingereza 'transgender' ni mtu mwenye hisia tofauti na maumbile yake ya asili, kama mwanaume anakuwa na hisia za kike kama mwanamke anakuwa na hisia za kiume na wengine wengi kubadili jinsia zao kabisa.
Wiki iliyopita Cleopatra Kamburu alikabidhiwa hati yake mpya ya kusafiria na kitambulisho chake, kikimtambulisha kama mwanamke.
Ameiambia BBC kwamba alikuwa na matumaini kitambo kwamba siku moja ingewezekana kutambuliwa. Lakini kupata hati na nyaraka hizo kulionekana kama hatua muhimu katika historia, sawa na wakati wanawake waliporuhusiwa kupiga kura kwa mara ya kwanza.
Alisema wakati hati yake ya kusafiria ilikuwa bado na herufi M (kwa maana ya kumtambua kama mwanaume), ilifika wakati ilimbidi avue nguo ili kuchunguzwa viungo vyake na kuthibitisha jinsia yake.
Anakumbuka siku moja tukio liliompomtokea: "Mtu mmoja aliniuliza, 'Wewe ni mwanaume au mwanamke?' lilikuwa jambo la aibu ... huna haja ya kuangalia sehemu za siri za watu kujua wao kina nani? "Tuna teknolojia ya kisasa ya 'biometriska' (teknolojia ya alama za vidole ama fingerprint au macho) kwenye mipaka. Nilimuuliza afisa wa uhamiaji, kama siwezi kutumia teknolojia hizo kujua mie ni nani.
"Kwa hiyo sikujua kwanini nililazimika kuchunguzwa viungo vyangu vya uzazi."