Zanzibar haina mgonjwa hata mmoja wa corona lakini yaonya kuhusu wimbi la tatu la maambukizi

Maelezo ya sauti, Tanzania inajiandaa na tishio la wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya Corona
Iliyochapishwa

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuwa kwa sasa visiwa hivyo havina mgonjwa hata mmoja wa Corona.

Kauli hiyo inakuja wakati ambapo Tanzania inajiandaa na tishio la wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya Corona. Zanzibar ikiwa sehemu ya Tanzania ni miongoni mwa maeneo barani Afrika yanayopokea wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani hivyo kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi hivyo.

Waziri wa Waziri wa Afya wa Zanzibar Mansor Mazrui amefanya mahojiano na mwandishi wetu Halima Nyanza.