Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wimbi la Panya kwenye mashamba lilivyosababisha hasara kwa wakulima
Iliyochapishwa
Vijiji vya nchini Australia vimekuwa vitani kupambana na ukame, moto wa nyika na mafuriko kwa miaka michache iliyopita.
Wakulima mwishowe walipata pumziko kwa kuwa na hali ya hewa nzuri iliyowapa mazao mengi.
Hali hizo pia zilikuwa kichocheo kwa panya, na idadi yao ililipuka katika sehemu za New South Wales.
Wakulima watatu wamezungumza na BBC kuhusu maisha ya kupitia pigo baya zaidi la wimbi la panya.