BBC Africa Eye :Fahamu Kwanini wastaafu wengi Nigeria wananyimwa pensheni zao
Iliyochapishwa
BBC Africa Eye imefanya uchunguzi wa siri na kuibua mfumo mbaya wa utoaji pensheni kwa rushwa nchini Nigeria,jambo ambalo linawaacha wazee kwenye maumivu na wagonjwa wakati kuna mafao yao ya kustaafu.
Mwandishi wa BBC Yemisi Adagoke ametembelea jimbo la Cross River State na kukutana na wastaafu ambao wamedaiwa kuwa wamekufa wakati wapo hai na hivyo kunyimwa haki yao ya mafao.
Baadhi yao wamelazimika kutegemea msaada wa kifedha kutoka kwa ndugu zao huku wakiwa wanaendelea kuhangaika kuiomba mamlaka kufuatilia madai yao ya pensheni.