Ratiba ya mazishi ya Rais Magufuli kutolewa leo

Maelezo ya sauti, Ratiba ya mazishiya Rais Magufuli kutolewa leo
Iliyochapishwa

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao Chatto, mkoani Geita.

Magufuli amefariki jioni ya siku ya Jumatano jijini Dar es salaam kwa matatizo ya moyo.

Msemaji wa serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas ameviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba, utaratibu wa maizishi yake na ratiba ya maziko utatolewa asubuhi hii na Makamu wa Rais wa Tanzania,Bi Samia Suluhu.