Hatua kuchukuliwa kwa watakaoongoza watalii wasiovaa mavazi ya stara
Iliyochapishwa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wageni na watalii kuzingatia miongozo ya maadili ambayo imekuwa ikitolewa na taasisi zinazosimamia Utalii.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imesema kuwa katika siku za karibuni kumekuwa na ukiukwaji wa mila, maadili na utamaduni wa Kizanzibari hasa katika suala la mavazi.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Lela Muhamed Mussa amezungumza na Scolar Kisanga kuhusu hatua hiyo.