Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Shule ya kwanza iliyojengwa kutokana na janga la corona
Iliyochapishwa
Wakati Santosh alipofika Neelam Thogu, kijiji kilicho katika misitu ya jimbo la kusini la Telangana nchini India, aliwakuta watu wanaoishi katika umaskini na watoto bila fursa ya shule.
Alikwenda huko na marafiki wawili kusambaza chakula na vifaa vya matibabu wakati wa janga la Covid-19.
Lakini waliishia kukaa na kuanzisha shule, ambapo watoto hujifunza Kiingereza na lugha ya mkoa wa Kitelugu.