Kamala Harris: Athari za kijamii na hisia kwa vijana wanaokua kwa mara ya kwanza na Makamu wa rais wa kwanza mwanamke wa Marekani

Kwa Harris kuchukua wadhifa wa makamu rais wa Marekani imechukuliwa kama hatua ya thamani katika historia ya taifa hilo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kwa Harris kuchukua wadhifa wa makamu rais wa Marekani imechukuliwa kama hatua ya thamani katika historia ya taifa hilo
Iliyochapishwa

"Masuala ya uwakilishi "ni mambo ambayo yamekuwa yakirudiwa mara kwa mara katika siku hizi nchini Marekani.

Watu wengi wanapozungumzia kuhusu ujio wa Kamala Harris katika kiti cha makamu wa rais wa nchi hiyo, wanauelezea kama wa kihistoria, karibu kila mmoja, akiuelezea kwa hisia kuu.

Una niña observa el discurso de Kamala Harris en televisión

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Harris atakuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa wa makamu wa rais , na pia mtu wa kwanza mwenye mweusi na mwenye asili ya Asia

Kamara Harris alikuwa Mwanasheria mkuu wa kwanza wa jimbo la California na Seneta mwanamke katika jimbo hilo.

Katika hotuba yake ya kwanza kama Makamu rais- mteule, Jumamosi iliyopita katika Delaware, kamera za televisheni zilikuwa zikikatiza picha zake jukwaani na kuonesha picha za umma uliohudhuria tukio.

Kamera ziliwamulika wasichana wadogo watatu wenye umri wa kati ya miaka 8 na 10 , waliokuwa mabegani mwa watu wazima, wakitabasamu na labda hawakufahamu umuhimu wa kile kilichokuwa kikiendelea.

Kamala Harris alitoa kauli za kuwashukuru wanawake walioweka historia kabla yake na alisema walikuwa mfano wa kuigwa na kizazi kijacho

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kamala Harris alitoa kauli za kuwashukuru wanawake walioweka historia kabla yake na alisema walikuwa mfano wa kuigwa na kizazi kijacho

Watakua wakimuona mwanamke katika kiti kikubwa zaidi cha pili muhimu cha kisiasa katika nchi na kwao litakua ni jambo la kawaida.

Kama Wendy Davis, mgombea wa kiti cha bunge la wawakilishi la Marekani Mdemocratic kutoka Texas aalivyoandika kwenye Twitter : "Ninafikiria kuhusu wasichana wote hao wadogo nchini Marekani na jinsi hii itakavyomaanisha kwao.

Wajukuu wangu wa kike watakua wakimuona mwanamke mwenye rangi katika White House na hawataona kuwa ni jambo lisilo la kawaida.

Inafurahisha kwangu mimi kufikiria kwamba hili litakuwa ni sehemu ya mambo 'ya kawaida' ''

Hiyo ndio maana ya kile ambacho wale waliodai umuhimu wa uwakilishi walikuwa wanamaanisha.

"Sitakuwa wa mwisho"

"Huku nikiwa ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huu, Sitakuwa wa mwisho ," Harris alisisitiza katika hotuba yake, na kuongeza kuwa : "Kwasababu kila msichana ambaye anatuangalia ataona kwamba hii ni nchi ambayo mambo yanawezekana."

Niña disfrazada de Kamala Harris

Chanzo cha picha, Twitter

Hotuba ya kwanza kama mtu aliyechukua wadhifa wake mpya iliibua gumzo kubwa miongoni mwa watu zaidi ya wanasiasa.

Mitandao ilifurika jumbe kutoka kwa akinamama na akina baba ambao walishirikishana athari za kihisia za kushuhudia wakati huu na kuweza kushirikishana pamoja na watoto wao kile kilichokuwa kikiendelea .

"Ni furaha iliyoje kwamba Makamu wa kwanza wa rais anaingia katika White House na pia ni mwanamke wa rangi ," mwanamuziki Ciara Wilson alimueleza binti yake mwenye umri wa miaka 3, Sienna, katika video iliyoshirikishwa mtandaoni mara elfu kadhaa.

"Binti yangu atapiga kura katika kipindi cha miaka 8 ijayo. Ninapoelezea kwamba huenda Kamala Harris akagombea kama rais nililia," aliandika mwanamke anayeitwa Quiana.

Una pareja escucha con emoción los discursos de Kamala Harris y Joe Biden en Delaware

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wasichana wengi walichagua kuvaa kama Kamala Harris katika sherehe ya Halloween

Meena Harris, mpwa wake makamu rais -mteule , ali tweet kwamba binti yake mwenye umri wa miaka 4 alisema : "'WASICHANA WEUSI WANAWEZA KUWA MARAIS! "

"Binti yangu mwenye umri wa miaka 11 na wasichana wote sasa wanaona nguvu ya uwezekano. Kutoka ndani ya moyo wangu ,Sina maneno ya kuwaelezea kile ambacho hii inamaanisha kwangu kama ," iliongeza mtumiaji mwingine wa Twitter.

Si wasichana tu

Umuhimu wa kukua ukimtazama mwanamke katika nafasi ya uongozi wenye mamlaka haiwaathiri tu wasichana, pia inaweza kushawishi mitizamo ya watoto kuhusu dunia.

Kwa baadhi, mazungumzo haya tayari yameanza kufanyikika.

Jennifer Richard, mkazi wa Miami, hafichi furaha yake kwa mwanae mdogo wa kiume juu , Kaden, mwenye umri wa miaka 13, juu ya kuchaguliwa kwa Kamala Harris.

Kamala Harris

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harris amechukua jukumu la uongozi , akitumia kipaza sauti kupaza sauti ambayo itaendelea kusikika

"Baada ya hotuba kutolewa, wakati droni zilipoandika jina la Biden angani, Kaden aliuliza haraka , ni lini wataandika jina Harris when are they going to write Harris? " anasema Jennifer.

"Na aliendelea kuuliza mara kwa mara hadi alipoona jina alilotaka kuliona limekuja ," aliongeza.

"Nilifurahi na kujivunia sana kwamba mwanamke amechaguliwa kama makamu rais…na mimi kama mama mtoto nilifurahi kwamba alitambua umuhimu wa wakati.

"Watoto wako wanaangalia kila mara. Waoneshe kitu kizuri ambacho wataiga ," alitahadharisha.

"Bw. Makamu Rais, Ninaongea "

Wakati wa mdahalo wake wa Makamu wa rais pamoja na Mike Pence, Harris alitoa moja ya kauli ambazo zitarekodiwa kama kauli zitakazokumbukwa zaidi za kampeni za uchaguzi .

Kamala Harris durante el debate vicepresidencial

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hotuba ya Kamala Harris ya Jumamosi ilisifiwa kwani ilionesha kuwa ni mtu aliyeamini kwa kile alichokizungumza.

"Bw. Makamu Rais, Ninaongea," Harris alimwambia Pence mara kadhaa alipojaribu kumkata kauli.

Kujiamini kulikoonekana katika sura ya mpinzani wake kisiasa , tayari kulikuwa kumedhihirika katika miaka yake katika Seneti, ambako alikuwa muulizaji mkakamavu wa wale waliokuwa wameteuliwa na Donald Trump katika nyadhifa mbali mbali , na pia amekuwa ni mfano wa kuigwa kwa wasichana na wanawake waliotaka kujitokeza.

"Kwa watoto wan chi yetu , haijalishi wewe ni wa jinsia gani, nchi yetu imetuma ujumbe wa wazi ," Harris alisema wakati wa hotuba yake .

" Uwe na ndoto zenye malengo, ongoza kwa imani na jione binafsi jinsi labda wengine wasivyo fahamu, ugfahamu kuwa tutakupongeza kwa kila hatua utakayopiga ."

Ujumbe huu unaonekana kuwa umeingia ndani ya mioyo ya wengi.

Section divider