'Saratani imenipokonya muelekeo wangu wa maisha'

Chanzo cha picha, INSTAGRAM / EMMYRHIANNON
Emmy mwenye umri wa miaka 29, amebobea kwa mambo ya urembo.
Alipatikana na saratani ya matiti akiwa mjamzito na amekuwa akishirikisha wengine changamoto anazopitia katika safari yake akiwa na matumaini ya kusaidia kina mama wengine vijana wanaopitia ugonjwa kama huo hadi kipindi cha kujifungua.
"Jana usiku nilipokuwa ninaosha nywele zangu nilitoa rundo la nywele kichwani kwangu. Sasa hivi nywele zangu ni nyembamba na zinang'oka zenyewe.
Awamu ya pili ya matibabu ya 'chemo', nilipoteza kope na nyusi zangu na hiyo imekuwa changamoto kubwa zangu.
Ni kipindi ambacho nalijiangalia kwenye kioo na kushindwa kujitambua.
Nilikuwa najihusisha na mambo ya urembo hadi hivi majuzi nilipolazimika kufunga kwa sababu imekuwa vigumu sana kijisimamia.
Lakini kinachonipa hamasa zaidi ni kufanya watu wahisi vizuri na ngozi zao. Hivyo basi kupoteza nywele nyusi zangu kumekuwa mapito magumu sana.
Sasa hivi nalazimika kujirembesha zaidi ili nionekane kama mwanadamu.
Sio tu kwamba mimi ni mama niliyepata mtoto karibuni ninayepigana na hisa zangu za kutaka kuwa vile nilivyokuwa kabla ya kuwa mjamzito, lakini sasa hivi mengi yamebadilika maishani mwangu.
Kwanza kabisa niliona uvimbe mnamo mwezi Mei nilipokuwa ninaoga. Kisha ukawa uko tu na hapo ndio nilipoanza kujiuliza maswali.
Baada ya siku chache nikaamua kumuona Lakini bahati mbaya kwasababu ya Covid-19 nilipoenda hospitali daktati alikuwa amevaa mavazi rasmi ya kujikinga na ikawa vigumu kwake kunifanyia vipimo kimamilifu.

Chanzo cha picha, INSTAGRAM / EMMYRHIANNON
Alinipa ushauri wa kuweka majani ya kabeji la baridi kifuani na kusema kuwa uvimbe umesababishwa na mabadiliko ya homoni kutokana na ujauzito.
Nikaondoka nikiwa nimeamini ushauri wa mtaalamu wangu.
Lakini baada ya wiki tano uvimbe huo ulikuwa umetanda hadi eneo zima la titi.
Ukawa unakua kweli na kulazimika kumuona daktari tena.
Baada ya kuona kuna kitu ambacho hakiko sawa, wakaamua kupiga picha mkono wangu wote pamoja na sehemu yake ya chini
Wakati huo nikiwa na ujauzito wa miezi 35, nikabaini kwamba nina saratani ya matiti.
Nilipata na mshtuko kweli.
'Saratani imenipokonya muelekeo wangu wa maisha'

Chanzo cha picha, INSTAGRAM / EMMYRHIANNON
Binti yangu, Brodie- Rey alizaliwa mapema kwa wiki tatu kupitia maji ua uchungu na pia nilifanikiwa kumnyonyesha mara moja tu.
Lakini siku ya pili madaktari walinipa matibabu ya kuzuia maziwa kutoka na sikuweza tena kumnyonyesha baada ya hapo.
Nilimaliza matibabu ya kemikali hivi karibuni na sasa naendelea kupata afueni nyumbani.
Niliarifiwa ratiba yangu ya matibabu baada ya mtoto kuzaliwa na kufahamishwa kuwa sitaweza tena kumnyonyesha.
Pia nilipewa dawa za kufanya hedhi kukoma ili kulinda mayai ya uzazi yasiathirike kutokana na tiba ya kemikali.
Na ikiwa mayai yangu ya uzazi hayatafufuka huenda nikapoteza uwezo wangu wa kuuza.
Kwa sasa hivi, pia najitahidi kutojiangalia kwenye kioo.
Lakini licha ya hayo yote kila ninapomuangalia mtoto wangu, huwa najiona mwenye bahati pamoja na jamii inayonizunguka ambayo imekuwa ikinipa msaada wa kipekee kwa kuniunga mkono.












