Jamii zinazokodisha ardhi yao kwa utalii mwaka huu waambulia patupu kutokana na corona

Maelezo ya sauti, Jamii zinazokodisha ardhi yao kwa utalii waambulia patupu
Iliyochapishwa

Jamii zinazoishi kwenye hifadhi za wanyama pori za kibinafsi nchini Kenya zina wakati mgumu kulisha familia zao huku athari za janga la Covid-19 zikiendelea kukithiri.

Katika hifadhi ya wanyama pori ya Maasai Mara, jamii hukodisha ardhi yao kwa wawekezaji na kulipwa kila mwaka, ada ambayo kwa mwaka huu wataikosa kwa sababu ya ukosefu wa watalii, na hivyo kuwasababishia hasara ya maelfu ya dola kwenye kambi za kitalii.

Mfumo huu wa uhifadhi huchangia kulinda wanyama huku utamaduni wa Kimaasai ukidumishwa pia.