Mwanaume aliyenaswa kwenye jengo lililoporomoka arekodi ujumbe wa kuhuzunisha

Iliyochapishwa

‘Ikiwa sitanusurika, buriani’ – mwanaume aliyenaswa kwenye jengo lililoporomoka arekodi ujumbe wa kuhuzunisha.

Khalid Khan alikuwa miongoni mwa raia walionaswa kwenye jengo la makazi la ghorofa tatu lililoporomoka huko Bhiwandi, viungani mwa Mumbai nchini India.

Bila ya mawasiliano ya simu, alijipata akirekodi video yake ya mwisho ya kumuaga mke wake. Lakini baada ya kukwama chini ya vifusi kwa saa 10, aliokolewa.