Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Anusurika kifo baada ya kupigwa mapanga mwili mzima na ndugu yake
Waswahili husema kikulacho ki nguoni mwako, mkulima mmoja kutoka Kisiwani Pemba, alinusurika kifo baada ya kupigwa na mapanga mwili mzima na ndugu yake ambaye alimkuta akimuibia ndizi shambani kwake.
Bwana Issa ni mkulima mdogo kisiwani Pemba wakati wa tukio hilo, aliigiza kama amekufa ili mwizi ambaye anatoka familia moja na yeye amuache.
Anasema anadhani alitaka kumuua kutokana na aibu ya kuja kufichuliwa kwamba alimkuta akiiba ndizi zake.
Issa ana shamba la mazao mbalimbali ikiwemo ndizi aina ya mkono wa tembo. Siku ya tukio alikua yeye na mtoto wa kaka yake wakichimba mihogo kwa ajili ya chakula cha nyumbani.
Mtoto huyo ndio aliyemsaidia kwa kukimbia kutoa taarifa ya tukio nyumbani.
Video: VSO/Justin Spray.