'Ilikuwa siku yenye furaha kubwa maishani kwangu'

Maelezo ya video, Harusi ya mgonjwa wa saratani aliyekuwa karibu kuaga dunia
Iliyochapishwa

Baada ya miezi sita ya kupambana na ugonjwa wa saratani, Tash Longhurst aliambiwa kuwa tiba anayopata haiwezi kumsaidia hivyo ana wiki kadhaa tu za kuishi.

Msichana huyo aliyekuwa na miaka 25-alikuwa na saratani ya nadra ifahamikayo kama 'spindle cell sarcoma' ambayo huwa inamfanya mtu kuwa na maumivu ya kifua.

Rafiki yake, Simon Young,alikuwa anasubiri muda muafaka kwa ajili ya kumchumbia na kumuoa lakini taarifa ya daktari iliwafanya waone si budi kusubiri tena.