Wanawake Afghanistan mara nyingi hulazimika kuficha majina yao hata wakiwa kwa daktari

Campaign poster for WhereIsMyName?
Maelezo ya picha, Kampeni iliyoanzishwa na wanawake miaka mitatu iliyopita, inataka wapewe haki yao ya kujitambulisha
Iliyochapishwa

Mwanamke ambaye tutampa jina la Rabia - kutoka magharibi mwa Afghanistan ana homa kali na akaamua kwenda kumuona daktari.

Daktari akabaini kwamba amepata maambukizi ya virusi vya corona.

Rabia akarejea nyumbani akiwa na maumivu makali na homa na kisha akatoa karatasi ya kununua dawa aliopewa na daktari na kumkabidhi mume wake ili amnunulie dawa.

Lakini punde tu baada ya mumewe kuona kwamba mke wake ameandikisha jina lake la kweli hospitalini, akashikwa na hasira na kuanza kumpiga kichapo cha mbwa akidai kwamba alifanya makosa kutoa jina lake kwa mtu ambaye hamjui.

Nchini Afghanistan, familia mara nyingi hulazimisha wanawake kuficha majina yao wanapokuwa nje.

Sahar Samet holding a poster promoting the WhereIsMyName? campaign

Chanzo cha picha, Sahar Samet

Maelezo ya picha, Sahar Samet anasema anadai kile ambacho ni haki yake ya msingi

Kampeni ya 'WhereIsMyName' ni nini?

Tatizo linaanza mapema pale msichana anapozaliwa. Inachukua muda mrefu kupewa jina.

Mwanamke anapoolewa, jina lake halitawekwa hata kwenye kadi ya mwaliko wa harusi. Anapokuwa mgonjwa, mara nyingi jina lake la ukweli linafichwa hasa akiwa ameenda kumuona daktari.

Na anapokufa, jina lake halitaandikwa kwenye cheti cha kifo au hata kaburini.

Hii ndio sababu wanawake wameanzisha kampeni ya kutumia majina yao kwa uhuru iliyopewa jina la "Where Is My Name?" yaani "Jina Langu Liko Wapi?" ambayo imesambaa sanaa kwenye mitandao ya kijamii.

'Heshima kwa kakangu, babangu na mchumba wangu'

Mwanamke mwingine kutoka eneo hilo hilo - alizungumza na BBC, ambaye pia hakutaka kutambuliwa au sauti yake itumike kwenye redio.

Yeye anaona hatua kama hizo zinazochukuliwa ni sawa.

Poster stating: We are not what other people define us (Sic). We have our own identity. Call me by my name. I am with #WhereIsMyName? I am with Laleh Osmany.

Chanzo cha picha, "Where is my name?" campaigners

Maelezo ya picha, Laleh Osmany limekuwa maarufu kwasababu ya kampeni ya WhereIsMyName?

Anasema: "Mtu anaponiomba nimwambie jina langu, ni lazima nifikirie heshima ya kaka yangu, baba yangu na mchumba wangu na nikifikiria kiasi hicho siwezi kusema jina langu.

"Kwa nini nikasirishe familia yangu, ? Je kuna maana yoyote ya kutaja jina langu?

"Nataka kutambulika kama binti ya baba yangu, dada ya kaka yangu. Na siku za usoni, nataka kutambulika kama mke wa mume wangu, kisha mama wa kijana wangu."

Top left, Afghan singer songwriter Ghezaal Enayat holding a sign saying 'Call me by my name' and other women campaigning for the WhereIsMyName? movement

Chanzo cha picha, Social media campaigns

Maelezo ya picha, Wanaharakati, ikiwemo mwanamuziki wa Afghan na mtunzi Ghezaal Enayat (kushoto), wameshika mabango kuhamasisha harakati zinazoendelezwa katika kampeni ya WhereIsMyName?

Simulizi kama hizi ni za kushangaza.

Kutumia jina la mwanamke hadharani haikubaliki na hata katika maeneo mengine ya Afghanistan, inaweza kuchukuliwa kama matusi au ukosefu wa heshima.

Wanaume wengi wa Afghan hawawezi kutaja majina ya dada zao, wake zao au mama zao hadharini kwasababu hilo linachukuliwa kama aibu au ukosefu wa heshima.

Kawaida wanawake huwa wanajulikana kama mama, binti au dada ya kaka mkubwa wa familia.

Sheria ya Afghan inasema kwamba jina litakalotumika pekee katika usajili wa cheti cha kuzaliwa kwa mtoto ni la baba peke yake.

Kina baba wasiotekeleza majukumu yao

Kando na matatizo yanayotokana na sheria hii, pia kuna athari za kihisia.

Farida Sadaat alikuwa bibi harusi mtoto aliyepata mwanawe wa kwanza akiwa na umri wa miaka 15. Yeye na mume wake walitengana na akahamia Ujerumani pamoja na watoto wake wanne.

Anasema kwamba mume wake hajawahi kuchukua majukumu ya watoto wao, ama kuwaangalia au hata kuwasalimia. Kwa hiyo anaamini kwamba mume wake hana haki ya majina yake kuwekwa kwenye vyeti vya kuzaliwa au vitambulisho vya watoto wao.

Farida Sadaat and her son

Chanzo cha picha, Farida Sadaat

Maelezo ya picha, Farida Sadaat alihamia Ujerumani na anasema kamwe hataruhusu majina ya mume wake ambaye hashughulikii watoto yajumuishwe kwenye vitambulisho vya watoto wao

"Nimekuza watoto wangu mwenyewe. Mume wangu alikataa kunipa talaka ili niolewe na mtu mwengine.

"Sasa basi, Nimekataa kabisa majina yake yawepo kwenye vitambulisho vya watoto wangu. Kuna wanaume Afghanistan ambao wana wanawake wengi, kama aliyekuwa mume wangu, na hawatunzi watoto wao.

"Natoa wito kwa rais wa Afghan abadilishe sheria hiyo na kina mama waruhusiwe kurekodi majina yao wakati wa kusajili cheti za kuzaliwa kwa mtoto na anapofikisha umri wa kupata kitambulisho."

Kampeni ikaanza

Laleh Osmay

Chanzo cha picha, Laleh Osmany

Maelezo ya picha, Laleh Osmay anasema alianzisha kampeni ya WhereIsMyName? kusaidia wanawake kupata “haki yao ya msingi”

"Hili haliwezi kuendelea milele," mwanamke wa Afghan, 28, alijiambia hivyo miaka mitatu iliyopita.

Laleh Osmany pia kutoka Herat, alifika mahali akachoshwa na sheria hiyo na hapo ndipo alipoamua kuanzisha kampeni ya WhereIsMyName? kusaidia wanawake kurejesha kile ambacho anasema ni "haki yao ya msingi".

Osmany ameiambia Idhaa ya BBC Afghan kwamba yeye na rafiki yake walitaka tu kuuliza swali hasa kwa wanawake wa Afghan kuhusu kwa nini wananyimwa utambulisho wao?

"Kampeni hii inaendelea kupiga hatua kiasi cha kukaribia kushawishi serikali ya Afghan kurekodi majina ya kina mama pia kwenye vyeti vya kuzaliwa vya watoto pamoja na majina ya baba," anasema.

Anafikiria kwamba Idhaa ya BBC Afghan ilifanya Maryam Sama, mbunge wa bunge la wawakilishi la Afghan, kuzungumzia kampeni hiyo bungeni?

Sama alitaka majina ya kina mama pia kurekodiwa kwenye vyeti vya kuzaliwa vya watoto na kuandika ujumbe kwenye Twitter kwamba kuna uungwaji mkono wa suala hilo kujadiliwa zaidi.

Maryam Sama checking her 2018 election campaign leaflets

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maryam Sama anaunga mkono kampeni ya WhereIsMyName? katika bunge la Afghan

Ukosoaji

Hata hivyo baada ya mahojiano ya shirika la BBC na Bi. Osmany kuwekwa kwenye mtandao wa Facebook, kuna baadhi ya maoni ambayo yalikuwa yanaunga mkono lakini wengine wakakosoa hoja hiyo.

Baadhi ya maoni yalikuwa yanamkejeli, na kutania kwamba siku za baadae atafanya kampeni ya kutaka majina ya jamii nzima kuongezwa kwenye cheti cha kuzaliwa.

Wengine walisema kipaumbele kinastahili kuwa kudumisha amani katika familia "Elewa mapendekezo unayoyapa kipaumbele" amesema mmoja wa wasomaji.

Wanaume kadhaa walimshutumu kuwa anataka majina yake yajumuishwe kwenye vitambulisho kwasababu hajui baba ya watoto wake.

Bi. Osmany anasema kwamba amekatishwa tamaa baada ya kuona kizazi cha vijana wenye uelewa mzuri, wanaweza kutoa maneno machafu kama hayo.