Virusi vya corona: Muziki watumika kuonyesha matumaini na upendo
Iliyochapishwa
Nesi mmoja raia wa Chile ambaye ni muuguzi wa wagonjwa wa corona ameamua kutumia muda wake wa ziada kuwapigia ala za muziki wagonjwa ambao ni mahututi kwa kutumia violin.
Nesi huyo huwa anawaburudisha mara mbili kwa wiki, majira ya saa 12 jioni.
Damaris Silva anapiga muziki maarufu wa Latin ili kuonyesha upendo na matumaini."Ninafanya hivi kutoka moyoni" anasema.