Je, Hussein Ali Mwinyi ndio alitarajiwa kuwa chaguo la CCM?
Iliyochapishwa
Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemchagua Dr Hussein Ali Mwinyi, kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho visiwani Zanzibar katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Dr Mwinyi, ambaye ni mtoto wa rais mstaafu wa awamu ya pili wa nchini Tanzania Ali Hassan Mwinyi, ni tabibu kitaaluma na waziri wa ulinzi wa sasa wa Tanzania.
Amewahi kushika nyadhifa zingine huko nyuma ikiwa ni pamoja na kuwa waziri wa afya na wa masuala ya muungano.
Mwinyi pia amewahi kuwa mbunge kote – Tanzania bara na visiwani.
Katika kujadili zaidi uteuzi huu wa Dr Mwinyi mwandishi wetu Sammy Awami amezungumza na mwandishi wa habari mkongwe na mchambuzi wa maswala ya Zanzibar Ali Sultan.