Jinsi rais Nkurunziza alivyowapanga marais Kagame, Kenyatta, Kikwete na Museveni

Iliyochapishwa

Mwanahabari wetu Salim Kikeke alimtembelea rais Pierre Nkurunziza na kufanya mahojiano naye mwaka 2015 kuhusu jinsi ambavyo angewapanga marais wenzake katika timu ya kandanda ya Afrika mashariki.

Mahojiano hayo yalifanyika kabla ya rais huyo kutangaza azma yake ya kuwania urais kwa muhula wa tatu, tangazo ambalo baadaye lilizua ghasia nchini humo.

Rais Pierre Nkurunziza alizikwa nyumbani kwake huko Gitega siku ya Ijumaa, baada ya kuugua kwa ghafla na kufariki.