Virusi vya corona: India yakumbwa na uhaba wa hospitali

Iliyochapishwa

Mji mkuu wa India, Delhi zaidi ya watu nusu milioni watapatwa na maambukizi ya virusi vya corona kufikia mwishoni mwa Julai, kulingana na maafisa.

Hata hivyo maambukizi mengi yameshuhudiwa katika mji wa Mumbai na hata kupita idadi iliyoshuhudiwa Wuhan, China ambapo maambukizi hayo yalishuhudiwa kwanza.

Hospitali nchini humo zimefurika na wagonjwa wengi wamefariki kutokana na ukosefu wa matibabu.