Kutoka maisha ya mtaani mpaka ubunifu wa bidhaa za pembe za ng'ombe

Jean Marie Vianney Habiyaremye anasema kuwa huwa wanatengeneza vifaa mbalimbali kwa kutumia pembe za ng'ombe.
Maelezo ya picha, Jean Marie Vianney Habiyaremye anasema kuwa huwa wanatengeneza vifaa mbalimbali kwa kutumia pembe za ng'ombe
Iliyochapishwa

Kwa wengi, pembe za ng'ombe zinafaa tu kwa kutupwa kwenye dangulo la takataka.

Lakini unaweza kukosa nafasi ya kubadilisha maisha ikiwa na wewe una maoni kama haya, kulingana na Jean Marie Vianney Habiyaremye mjasiriamali kijana kutoka Rwanda aliyekuwa mtoto wa mitaani na ambaye sasa amezifanya pembe za ng'ombe kuwa "biashara yake kubwa" kwa kutengeneza vifaa mbali mbali pamoja na mapambo kutokana na pembe za ng'ombe.

Mwandishi wa BBC Kigali, Yve Bucyana alimtembelea kijana huyo katika karakana inayotengeneza pembe za ng'ombe ya ''Cow Horns Rwanda''

''...Pembe.. tunatengeneza kifaa hiki kwa kuweka pembe mbili ambazo zimechorwa sawasawa na kufanya pambo zuri sana la mahali kama ofisini'.'

Jean Marie Vianney Habiyaremye anasema huwa wanatengeneza vifaa mbalimbali kwa kutumia pembe za ng'ombe.

'Mfano ni kama tunataka kutengeneza sahani ,tunachemsha mafuta kisha tunaweka kwenye mashine pia pembe tunaiweka ndani.

bidhaa za pembe za ng'ombe
Wanatengeneza vifaa kama sahani, vijiko ,vikombe na aina mbalimbali za mapambo ya mwili kama hirini ,mikufu ,pete nakadhalika na pia mapambo ya nyumbani na ofisini.
Maelezo ya picha, Hereni, mikufu ,pete ni miongoni mwa bidhaa zinazotengenezwa na pembe za ngombe

Mchanganyiko huo unaifanya pembe kuwa laini sana kiasi cha kuweza kuivuta tunavyotaka kwa kutumia mikono kufuatana na umbile la kifaa tunachotaka kutengeneza.''

Wanatengeneza vifaa kama sahani, vijiko ,vikombe na aina mbalimbali za mapambo ya mwili kama hereni ,mikufu ,pete nakadhalika na pia mapambo ya nyumbani na ofisini.

Jean Marie Vianney Habiyaremye
Maelezo ya picha, Jean Marie Vianney Habiyaremye akiwa na wenzake

Bwana Habiyaremye mwenye umri wa miaka 28 alikuwa mtoto aliyekulia maisha ya mitaani.

Binti huyo anasema kuwa hata yeye hajaamini macho yake jinsi maisha yake yalivyobadilika:

''Nilikuja Kigali kutafuta kazi nilikuwa mtoto mdogo sana.

Kazi niliikosa nikaamua kuwa mzululaji ama mtoto wa mitaani sababu sikutaka kurudi kijijini.

Baada ya muda tulipata msamaria mwema kutoka Japan aliyekuwa na shirika la kuwasadia watoto wa mitaani akatufundisha kutengeneza pembe za ng'ombe ''

Kazi hiyo ndiyo biashara yake na sasa, na yeye ni miongoni mwa wajasiriamali vijana anayeweza kutoa ajira kwa vijana wenzake.

bidhaa
mapambo

''Mtaji wangu ulikuwa faranga elfu kumi na saba sasa mimi ni milionea , niliweza kununua ardhi na kujenga karakana hii kwa milioni 6 pamoja na hizi mashine unazoona hapa.

Yote haya yanagharimu franga zaidi ya milioni 13 na sasa najaribu kukarabati na kutanua mradi wangu.

Kadhalika nina watumishi zaidi ya 14 ambao kila mwezi wanalipwa mshahara.

Ni miaka mitatu tangu nianze sijapata hasara yoyote katika biashara yangu hii.''

Pamoja na hayo Habiyambere anasema bado wana matatizo ya kutumia mashine ambazo siyo za kisasa katika sehemu kubwa ya kazi yao wakilazimika kutumia mikono.