Mapacha ambao walitenganishwa na ubaguzi wa rangi

Iliyochapishwa

Margaret as a young woman

Chanzo cha picha, Nathan Romburgh

Miongo kadhaa baada ya kupata dharura ya afya Nathan Romburgh na dada zake waliangalia historia ya familia yao, na kujiuliza kuhusu siri iliyopo katika uasili wao.

Tarehe 29 Septemba 1969, mjini Cape Town, majira ya saa nne usiku, mji wao ulikumbwa na tetemeko la ardhi. Margaret Buirski anafanya kazi ya uuguzi katika kitengo cha huduma ya kwanza huko Alhambra , wa mara ya kwanza huduma ya utaalamu wake ilionekana kuhitajika sana . Wakati ambao mwanamke alianguka kutoka juu ya veranda la jengo na Margaret aliweza kumuhudumia majeraha aliyopata katika ajali hiyo.

Mwanaume mmoja mdogo aliyekuwa amelewa sana aliweza kubaini kuwa muuguzi huyo kuwa ana miguu mizuri. Licha ya kwamba alikuwa amelewa sana lakini bado alitaka kumpa lifti ya kumpeleka hospitali.

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa mahusiano ya kimapenzi kati ya Margaret na Derek Romburgh.

Margaret akiwa katika mavazi yake ya unesi amesimama nyuma ya gari la dharura la St John

Chanzo cha picha, Nathan Romburgh

Maelezo ya picha, Margaret akiwa katika mavazi yake ya uuguzi amesimama nyuma ya gari la wagonjwa la St John
Presentational white space

"Mara zote walipokutana walikuwa wanakumbushana kuwa walikutana katika janga la tetemeko la ardhi," alisema Nathan Romburgh, 42, ambaye ni mtoto wao mdogo. Alimuelezea mama yake kama muhusika . Aliweza kujizungumzia mwenyewe kuhusu kazi yake na baadae kuondoka, alisema.

Ndoa yao haikuwa ya furaha. Derek aliendelea kunywa pombe na walikuwa na kipato kidogo sana.

Margaret aliweza kukabiliana na tatizo hilo bila mafanikio, na kuwaambia watoto wake kuwa walikwa matajiri sana, jambo ambalo watoto hawakuliamini.

Nathan na dada zake - Bernadette na Shereen - hawakujua nini kilimpata mama yao na hawakuwahi kujua kuhusu familia iliyomuasili.

Walifahamu kuwa walimuasili mtoto mwenye asili ya kiyaudi ambaye alikufa akiwa kijana mdogo.

Familia ilimtenga pale alipoamua kuoana na Derek, ambaye hakuwa kabila lake. Licha ya kwamba, Margaret alikuwa anajivunia sana asilia wake.

Mzazi aliyemuasili Margaret alikufa wakati akiwa binti mdogo

Chanzo cha picha, Nathan Romburgh

Maelezo ya picha, Mzazi aliyemuasili Margaret alikufa wakati akiwa binti mdogo
Presentational white space

Nathan hakuwa na mahusiano mazuri na mama yake na wakati wazazi wake walipoachana mwaka 1991, aliamua kutoishi naye na kwenda kuishi kwa bibi.

"Siwezi sema uongo - hakuwa mama mzuri kabisa," alisema.

Bernadette, Nathan na Shereen walipokuwa kwenye harusi ya wazazi wao

Chanzo cha picha, Nathan Romburgh

Maelezo ya picha, Bernadette, Nathan na Shereen walipokuwa kwenye harusi ya wazazi wao
Presentational white space

Miaka mitatu baadae, wakati Margaret alipokuwa anakabiliana na ugonjwa wa saratani , alitangaza kuwa na dada.

Nathan alipuuzia na kudhani kuwa ni simulizi nyingine za uongo za mama yake za tangu mwaka 2008 wakati dada yake mkubwa Bernadette alipopata saratani ya matiti.

"Anasema jambo hilo lilikuwa linatisha sana ," alisema Nathan. "Hivyo tuliamua kufuatilia asili ya mama yangu ili kujua vinasaba vya watu wa huko.

Nathan na dada yake Shereen waliamua kusaka taarifa zaidi kuhusu historia ya familia yao.

Bernadette, Nathan na Shereen katika harusi ya Nathan

Chanzo cha picha, Nathan Romburgh

Maelezo ya picha, Bernadette, Nathan na Shereen katika harusi ya Nathan

Jambo la kwanza ambalo Nathan alilifanya ni kuomba cheti cha kuzaliwa cha Margaret. Na kiliwashangaza sana.

Jina la mama yao lilikuwa Mary Magdalena Francis, jina ambalo wanalitumia zaidi wakatoliki.

"Hivyo tukagundua kuwa bibi yetu hakuwa Muyahudi," alisema Nathan.

Wakati wanaendelea kufuatilia historia ya familia yao, waligundua kuwa walikuwa na asili ya Uhispania. Na vilevile alifahamu kuhusu Alan Francis ambaye walidhani kuwa ni ndugu yao.

"Nadhani tutakuwa na undugu," alisema.

"Tulifahamu kuwa alikuwa na kashfa mara nyingi!"

"Maisha yangu yote, nilimjua kuwa mtu ambaye hasemi chochote " alisema Alan, 77.

"Shangazi Mary alikuwa anasema hivyo kwangu: 'Nitakwambia nikiwa kaburini, Mungu ambariki kwa sababu hakuwahi kuniambia."

Mary Magdalena Francis - bibi yake Nathan - alifariki kwa ksaratani mwaka 1998 - miaka minne baada ya mtoto wake kufariki kutokana na tatizo la saratani.

Na Nathan aligundua kuwa mama yake alikuwa anasema ukweli kuwa alikuwa na dada. Jina la dada yake lilikuwa ni Norma. Lakini yeye pia alifariki na ugonjwa wa saratani mwaka 2006.

Alan alifahamu kuwa Mary aliishi Afrika kusini na bosi wake ambaye alikuwa daktari aliyekuwa na ndoa yake na watoto ndio alimpa ujauzito . Baadae, Mary aliolewa na kuhama.

Siri ambayo Mary alikufa nayo ni kusema ukweli kuwa alijifungua watoto wawili lakini alimtunza mmoja tu.

Norma akiwa na wazazi wa Alan Francs

Chanzo cha picha, Alan Francis

Maelezo ya picha, Norma akiwa na wazazi wa Alan Francs

Nathan alihuzunika sana kujua kuhusu taarifa hiyo baada ya miaka mingi kupita.

Mary alihamia Uingereza na baadae kuolewa. Na sasa anatumia jina lake la Bwana yake.

Huu ulikuwa wakati ambao aligundua kuhusu uasili wake: Shangazi yake Norma na mama yake walikuwa wanasheherekea siku moja ya kuzaliwa.

Na Mary hakumwambia siri yake kuwa alizaa watoto mapacha na kumlea mmoja.

"Hilo ndio swali lake kubwa - jambo gani linaweza kumfanya mtu amgawe mwanae, ni vigumu kuelewa," alisema Nathan.

"Mama yangu alikuwa na rangi ya nyeusi, lakini aliweza kuishi na watu weupe wakati wa ubaguzi nchini Afrika kusini," alisema Nathan. "sidhani kama Norma angeweza."

Mary Francis, bibi yake Nathan alikuwa ametoka Ulaya, alikuwa chotara. Baba yake Mary, James Francis, alikuwa Muingereza na mama yake, Christina, alikuwa ana asili ya Malasia. Mary alikuwa mdogo kuliko wote kati ya watoto sita.

James Francis,akiwa na mke wake Christina Leonora na watoto wake watatu - Nora, Percival na Mary

Chanzo cha picha, Alan Francis

Maelezo ya picha, James Francis, akiwa na mke wake Christina Leonora na watoto wake watatu - Nora, Percival na Mary
Presentational white space

Wakati wakoloni wakwanza walipowasili, mahusiano ya mchanganyiko wa rangi yaliibuka Afrika Kusini na wanawake wa kabila ya Khoisan na Xhosa, pamoja na wanawake waliotoka Malaysia au St Helena, ambao waliletwa kama watumwa.

Lakini baada ya chama cha National Party kilipoanzishwa mwaka 1948, sheria kadhaa kusema kuwa mahusiano ya namna hiyo ni kinyume na sheria.

Sheria iliwekwa kuwa ni marufuku kwa watu watu kutoka ulaya ni marufuku kuoa au kuolewa na watu ambao hawajatoka ulaya na sheria hiyo ilianza kutekelezwa Julai, 8,1949-mwezi mmoja kabla mapacha hao hawajazaliwa.

Sheria hiyo ilienda mbali zaidi mwaka 1950, ambapo walipiga marufuku wa watu ambao wana asili tofauti kuwa na mahusiano ya kingono na kuwataka kila mtu kujiandikisha kama yeye ni 'mwafika', 'mzungu' au 'mhindi'.

Viwango hivyo uasili wa watu vilipimwa kutokana na picha na muonekano wako, vilevile walikuwa wanatumia kalamu ya risasi maarufu ambayo ilikuwa inawekwa kwenye nywele kujua ni za mtu wa asili gani.

Lakini watu wenye mchanganyiko wa asili wanaweza kuwa na muonekano tofauti hata kama wametoka familia moja.

Hivyo inawezekana hakuwa na namna nyingine - ndio maana familia ya kiyaudi walikubali kumuasili Margaret na kumkataa Norma kwa sababu hawakutaka kuwa na mtoto ambaye anaonekana tofauti na wao.

Au inawezekana walikuwa wanataka mtoto mmoja na sio wawili.

Lakini Nathan aliamini kuwa Mary alikuwa anaenda kuwa na maisha bora zaidi kuliko angemlea yeye.

Wakati wa ubaguzi wa rangi , watu waliokuwa wamechanganya uasili wao walikuwa wanapata wakati mgumu zaidi.

Ubaguzi ulikuepo kwenye maisha ya kila siku, kwa kuangalia eneo ambalo wanaishi, usafiri wa umma na shule pamoja na hospitali ambazo wanatumia.

Ubaguzi wa rangi katika usafiri wa umma

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Ubaguzi wa rangi katika usafiri wa umma
Presentational white space

Matokeo ya ubaguzi huo yaliifanya familia kutengana au kutambuliwa tofauti.

Alan Francis anasema anakumbuka vizuri namna alivyokuwa anabaguliwa kutokana na rangi yake kuwa nyeusi huku dada yake alikuwa sio mweusi sana na nywele zake zilikuwa za rangi ya udongo.

Dada yake alikuwa anapata kipato kikubwa kwa sababu alikuwa anafanya kazi na watu weupe.

Mwaka 1950 wazazi wa Alan walihamia Uingereza na ndugu zake wengi Francis walihamia huko. Mary alihamia huko pia mwaka 1956, na mtoto wake aliyekuwa na miaka saba- Norma.

Mary alipata kazi katika shirika la usafiri mjini London na kuolewa na mhandisi. Mama na binti yake waliishi pamoja kwa muda wote.

Mary na mume wake George akiwa kwenye basi mjini London

Chanzo cha picha, Crispin Belcher

Maelezo ya picha, Mary na mume wake George akiwa kwenye basi mjini London

Lakini Norma hakuwahi kufahamu kuwa alikuwa na pacha wake nchin Afrika kusini?

Inaonekana kuwa miaka ya nyuma ambayo Margaret alikuwa anajaribu kuwasiliana na watu kujua kuhusu familia yake lakini hakuna aliyejibu.

Wakati walikuwepo watu waliojua kuhusu uwepo wa ndugu yake.

Norma, Mary's husband George and Mary

Chanzo cha picha, Crispin Belcher

Maelezo ya picha, Norma Francis, George: mume wake Mary na Mary
Presentational white space

Norma mwenyewe hakujua ukweli kuhusu historia yake, kwa mujibu wa rafiki zake ambao walikuwa wanamuhudumia wakati anaugua saratani.

From left: Norma, Mrs Belcher Mary Francis, Mary Belcher

Chanzo cha picha, Crispin Belcher

Maelezo ya picha, Norma na Mary wakiwa na mama yake Crispin na dada yake mwaka 1980s

Nathan alianza kumuonea huruma mama yake baada ya kugunua ukweli alipoanza kufuatilia kuhusu uasili wake.

Anasema alikuwa anajivunia sana uasili wake ndio maana aliweka matumaini ya kuwapata ndugu zake ambao wametoka katika upande mwingine wa familia.

Nani ni nani?

Nathan, Bernaditte na Sheeran ni watoto wa Margaret Buirski na Derek Romburgh. Margaret aliasiliwa akiwa mtoto.

Mama yake mzazi alikuwa akiitwa Mary Francis.

Mary Francis alikuwa na mtoto mwingine wa kike, aitwae Norma, ambaye ni pacha wake Margaret.

Norma alilelewa na Mary na kuhamia mjini London.

Baba mzazi wa mapacha hawa alikuwa daktari ambaye alikuwa na familia yake nyingine, alijulikana kama Dkt Joshua.

Nathan na ndugu zake waliweza kuwagundua ndugu wengine kutoka familia ya mama yao, wakiwemo binamu Alan, Roy na Nora Francis.

Nathan pia aliweza kuwasiliana na mmoja wa watoto wa Dkt Joshua, ambaye ni kaka anae changia mmoja wa wazazi na mama yake Nathan, ambaye anageuka kuwa mjomba yake Nathan.

Nathan aliwasiliana na mtoto huyo kwa kutumia mtandao wa facebook, na kuweza kuzungumza usiku huo huo.

Ingawa hakuwa najua kitu chochote kuhusu uwepo wa Norma na Margaret, mtoto huyo wa daktari hakushangaa sana kusikia kuwa kuna uwezekanao ya kwamba baba yake anaweza kuwa na watoto wengine nje ya familia yao.

Presentational grey line

''Aliniambia kuwa baba yake alikuwa ni mtu ambaye anapenda sana wanawake,'' alieleza Nathan.

Alizungumza na mwanaume huyo ambaye alikuwa anaombea awe mjomba yake, kwa muda mrefu, huku kila mtu akijifunza kitu kutoka kwa mwenzake.

''Ilichukua muda sana kwa yeye kutambua kuwa mimi ni mpwa wake, nilijua pale alipojua tu akasema 'Aha!' kwa shauku sana.''

Alimwambia Nathan kuwa baba yake alikuwa ana uhusiano mkali na jamii ya matibabu ya kiyahudi mjini Cape Town, kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa sana kuwa yeye ndiye aliyepanga kuasiliwa kwa Margaret.

Unaweza pia kusoma:

Lakini, alimueleza kuwa Dkt Joshua hakuwa myahudi, alitokea katika jamii ya watu wa rangi wa Cape Town, huku akiwa anauwasili wa kutokea St Helena.

Mtoto wake alimwambia Nathan kuwa sababu za wazazi wake kuondoka Afrika kusini ni mada nyeti.

Mke wa Dkt Joshua alikuwa muingereza, walikutana alipomaliza mafunzo yake ya udaktari nchini Uingereza.

Presentational grey line
Presentational grey line
Presentational white space

"