Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rouhani amjibu Trump na kusema ni adui wa Iran
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema rais wa Marekani ni adui mkuu wa taifa hilo kuanzia utosini hadi kwenye unyayo. Ameyasema hayo akijibu ujumbe wa rais Trump alioutoa kupitia ukurasa wake wa twitter.
Katika ujumbe wake rais Trump amesema kuwa waandamanaji wa Iran wanadai haki yao ambayo wamekuwa wakipigania kwa miaka mingi kuhusiana na njaa na kukosekana kwa uhuru wao.
Picha za video zimeonyesha waandamanaji wakikabiliana na Polisi katika maandmano yaliyoanza tangu siku ya alhamis na ambayo yanaendelea katika kusambaa katika miji mingine nchini humo.
Polisi mmoja ameuawa na waandamanaji hao ambao baadhi yao wanajihami kwa bunduki aina ya rifle na hivyo kufanya idadi ya watu 13 kuuawa hadi sasa.